Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameibeba sekta ya kilimo kwa mafanikio makubwa sana katika miaka 4 ya utawala wake kwa kuhamasisha watu wengi zaidi kujihusisha na kilimo na kuvutia wawekezaji.

Akiongea kuhusu mafanikio hayo, Mtaka amesema kuwa katika kipindi hicho, sekta ya kilimo imepiga hatua kubwa sana ya maendeleo ikiwemo taasisi za kifedha na mabenki kutoa mikopo ya riba nafuu ambayo kwa kiasi kikubwa imeinua sekta ya kilimo na kuwainua wakulima.

“Rais Samia amefanya mageuzi makubwa sana kwa kwenye sekta ya kilimo na mnyororo wake wa thamani ambapo alielekeza taasisi za kibenki kuweza kutoa mikopo ya kilimo kwa singo digit ( asilimia 9 ),”

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Uhifadhi wa Chakula nchini (NFRA) wakifuatilia kwa makini moja ya wasilisho kwenye kikao cha Bodi hiyo jijini Arusha hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine Bodi hiyo ilipitia na kuujadili Mpango Mkakati wa miaka mitano wa NFRA. Kushoto ni Bw Anthony Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,katikati ni Bi Chabu Mishwaro na kulia ni Bw Robinson Meitikinyiku.

“Hivi sasa kupitia mageuzi haya tunashuhudia kwa mara ya kwanza sikio la mkulima linasikilizwa na taasisi za kibenki kutoa mikopo ya riba na masharti nafuu,”, amesema Mtaka.

Amesema katika miaka ya nyuma, Serikali iliwahamasisha wakulima wapime ardhi kwa njia mbalimbali ikiwemo za asili ili waende katika mabenki na taasisi za kifedha kwa ajili ya kukopa pesa na jambo hili halikuwa na mafanikio sana,”

Lakini hivi sasa kwa mazingira yaliyopo, taasisi mbalimbali za fedha na mabenki kama vile Benki ya Maendeleo (TIB) zinawafuata wakulima na kutoa riba ili waweze kujiendeleza katika kilimo.

Amesema kuna wakulima, wavuvi na wafugaji wakiwemo wa Ng’ombe wa Maziwa ambao wamepata mikopo ya riba nafuu ambapo hivi karibuni wakati Rais Samia akiwa Mwanza alizindua vizimba vya Samaki kwa wakulima waliopata mikopo ya riba nafuu.

Akitolea mfano katika mkoa wake wa Njombe, Mtaka ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) amesema benki za CRDB na NMB zimekuwa zikiwakopesha wakulima wanaolima mazao ya muda mfupi kama vile viazi na sasa wanaangalia uwekezano wa kuwakopesha wakulima wanaolima mazao ya muda mrefu likiwemi zao la Parachichi.

“Haya ni mageuzi makubwa sana ya Rais Samia katika sekta ya kilimo katika kipindi chake cha miaka minne akiwa madarakani,” amesema.

Kupitia kilimo, Mtaka amesema kuwa Rais Samia kwa mafanikio yanayopatikana katika sekta ya kilimo ameonesha matamanio yake ya kutamani kuiona Tanzania inakuwa tegemeo kubwa la chakula barani Afrika.

“ Hii inatokana na uwekezaji na uwezeshaji ambao Rais Samia ameufanya kwa NFRA ( Wakala wa Uhifadhi wa Chakula nchini) ambapo tumeweza kuhifadhi nafaka za chakula za kutosha kwa usalama wa nchi na kuuza maelfu ya tani ya mazao ya ziada nje ya nchi zenye uhitaji wa chakula na kuiingizia nchi fedha za kigeni,” amesema.

Mtaka amesema kuwa NFRA , mafanikio iliyoyapata inatoka kwenye kununua tani laki 4 hadi kufikia tani milioni 1 za mahindi kutoka kwa wakulima ambapo mabenki yanaikopesha taasisi hiyo ili iweze kununua nafaka kwa wingi na kumuwezesha mkulima kuona tija na faida ya kilimo chake.

Amesema mageuzi haya yamesababisha mazao kama vile Mahindi kuwa mazao ya biashara badala ya mazao ya chakula kama ilivyozoeleka hapo zamani.

“Miaka 10 iliyopita tukiwa shuleni tulijifunza kuwa mazao haya ni mazao ya chakula, lakini baada ya mageuzi mbalimbali kufanyika, mazao haya hivi sasa yamekuwa na tija kibiashara kwa wakulima,” amesema.

Amesema Serikali ya Rais Samia imekuwa ikitumia jitihada mbalimbali katika kuwainua wakulima wa mazao mbalimbali kama vile mpunga na viazi mviringi kwa kutoa ruzuku katika mbolea na pembejeo na kuwapa mashamba darasa .

“Kwa kufanya hivi, Serikali inasaidia kuinua hali za wakulima kiuchumi kwa sababu wakulima wanapata mahitaji yao mfano mbolea kwa gharama nafuu,”

Amesema Serikali imekuwa ikifanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo ambapo hivi karibuni Waziri wa Kilimo (Hussen Bashe) ameelezea bungeni utaratibu wa kuwafikia wakulima wadogo wadogo kwa kuwachimbia visima na kuwawekea miundombinu ya umwagiliaji ili kukuza sekta hii .

“Tunauona uwekezaji mkubwa wa kilimo ukiendelea kufanyika hapa nchini,” amesema.
Amesema miradi mbalimbali ukiwemo wa ‘Building a Better Tomorrow’ inayofanywa na Wizara ya Kilimo