Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanal Evans Alfred Mtambi ametoa wiki Sita kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kukamilisha Bweni la wanafunzi wakidato cha tano katika shule ya sekondari Ngoreme lilojengwa kwa nguvu za Wananchi na wanafunzi waliosoma katika shule hiyo.

Mtambi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara Wilayani Serengeti Mkoani humo ambapo shule hiyo tayari imepangiwa wanafunziambao kwa sasa wanalazimika kulala kwenye madarasa mawili hivyo kumlazimu kuagiza kukamilisha Bweni hilo ili lianze kutumika.

Bweni hilo la wanafunzi wa kidato cha tano lilijengwa na kuwekewa jiwe la msingi mwaka 2017 kwa gharama ya shilingi milioni 78  

Please follow and like us:
Pin Share