Na Mussa Juma, JamhuriMedia, Babati

Mkuu wa Mkoa Manyara, Qeen Sendika ametaka sekta ya michezo mkoa Manyara kuendelea kutumika katika kukuza Utalii na uhifadhi wa mazingira na wanyamapori.

Sendeka alitoa agizo hilo katika fainali ya michuano ya Chemchem CUP 2024 ambayo ilikuwa na kauli mbiu ya Ukoa Twiga,tunza Mazingira.

Katika fainali hiyo,timu ya Majengo FC imefanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kucharaza timu ya bodaboda FC magoli 2-1.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi za washindi, Mkuu.huyo mkoa alisema michezo ina fursa nzuri ya kukuza utalii na kutokomeza ujangili.

Alisema Michuano ya chem chem CUP ambayo hufanyika kila mwaka, imeonesha mafanikio mazuri ya kukuza uhifadhi na kuleta mahusiano mazuri na jamii.

“Serikali mkoa Manyara inapongeza kazi nzuri ya chem chem na tumekuwa tukifatilia michuano hii imekuwa na manufaa makubwa”alisema

Alisema wakati wa uzinduzi mwaka huu hakufika lakini alimtuma mkuu wa wilaya ya Mbulu,Veronica Kessy kumwakilisha lakini kwenye fainali ameamua kushiriki mweyewe kutokana na kutambia umuhimu wa michezo.

Mabingwa wa michuano hiyo, walikabidhiwa kikombe na fedha taslimu kiasi cha sh 2.5 millioni ,huku mshindi wa pili akipata zawadi ya sh 1.5 milioni na mshindi wa tatu Maklayoni FC akipata zawadi ya sh 1 milioni.

Kwa upande wa timu za Vijana chini ya miaka 18 wa mkoa alikabidhi zawadi ya kikombe ya fedha taslimu million Moja kwa mabingwa Maweni FC na mshindi wa pili alikuwa Kakoi FC aliyepata sh 600,000 huku mshikemshike FC akiwa wa tatu na kuzawadiwa 400,000.

Kwa upande wa wasichana Upengo Queen ya Olasiti waliibuka mabingwa na kuzawadiwa sh1.5 milioni na Mdori queen walikuwa wa tatu wakizawadiwa million Moja.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Babati Anna Mbogo alisema mashindano hayo yamesaidia sana kupunguza ujangili wilayani Babati na kuendeleza utalii.

Mbogo alisema Sasa vijana wengi wa Burunge WMA wamekuwa mabalozi wazuri wa utalii na Uhifadhi kwani manufaa wanayaona ya kutunza wanyamapori.

Mwenyekiti wa Burunge WMA, Erick lilayani alisema alisema mashindano ya chem chem CUP yameimarisha uhifadhi na kukomesha ujangili katika eneo la Burunge.

Alisema Burunge WMA inapongeza Taasisi ya Chem chem kwa kuendelea kuendesha mashindano hayo na Kila mwaka yamekuwa. yakivutia watu wengi.

Kwa upande wa Meneja mahusiano wa Chem Chem Charles Sylivester alisema lengo la michuano hiyo ni kushirikisha jamii katika uhifadhi wa mazingira na kupiga vita ujangili kupitia michezo.

Jumla ya timu 35 zimeshiriki michuano ya Chem chem CUP mwaka 2024 kutoka vijiji 10 ambavyo vinaunda hifadhi ya jamii ya Burunge wilayani Babati mkoa Manyara.