Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Septemba 1, 2023 ametoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari katika Ukumbi wa Mikutano JNICC kuhusu kufanyika kwa Kongamano la mifumo ya Chakula Afrika (AGRF SUMMIT 2023- Tanzania) Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere (JNICC)
RC Chalamila akiongea na Waandishi wa Habari amewataka wakazi wa Mkoa huo na Watanzania wote kwa Ujumla kutumia nafasi hii vizuri kwa ajili ya kujipatia uzoefu na ujuzi katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, Biashara uwekezaji na kujifunza matumizi ya Teknolojia za Kisasa Katika kufanya kazi hizo kwa urahisi na tija na hatimaye kufikia malengo ya nchi na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuzalisha mazao ya kutosha na ziada kulisha Afrika na ikibidi Dunia lakini pia kutekeleza ajenda ya Dunia ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayozidi kuongezeka siku hadi siku kote Duniani ili kwa pamoja tuweze kunusuru nchi yetu.
Aidha RC Chalamila amesema Mkoa wa Dar es Salaam umebahatika kuwa mwenyeji wa jukwaa la Mkutano wa mifumo ya Chakula Afrika 2023 litakalo anza tarehe 4-8 septemba 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC ambako Uzinduzi wake ulifanyika Ikulu ya Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania machi 7,2023 na kilele cha Kongamano hilo kitakuwa septemba 7,2023 siku ya Alhamis kuanzia saa 4:00 Asubuhi
Jukwaa la mifumo ya Chakula Afrika pamoja na mambo mengine ni jukwaa linalojadili maendeleo ya kilimo na Usalama na mifumo ya chakula barani Afrika, hii ikiwa ni mara ya pili nchi yetu inabahatika kuwa mwenyeji, hadi kufikia leo ma Rais 5 wa nchi za afrika wamethinitisha kuhudhuria na watu takribani 2000 wamejisajili kishiriki Mkutano huo, kupitia vyombo Habari Mhe Chalamila ameuhakikishia umma kuwa Mkoa uko tayari kuwapokea Viongozi na wageni wote watakaoshiriki katika Kongamano hilo, pia umejipanga vizuri katika masuala ya usalama, Malazi na huduma mbalimbali kulingana na Mkutano huo.
Mwisho Mtendaji Mkuu wa JNICC Bwana Ephraim Mafuru amesema maandalizi ya Mkutano huo hadi sasa yamekamilika katika nyanja zote.