Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema biongozi wa dini wanawajibu mkubwa katika jamii katika kuleta maendeleo na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo Septemba 14, 2023 katika ukumbi wa mikutano Yombo unaomilikiwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakati wa kongamano kubwa la dira ya uamusho wa miaka 13 ya TAG.
Kupitia kongamano hilo amesema lina bainisha dhana hiyo kwa sababu kazi mojawapo ya uamusho ni uinjilishaji kwa maana ya kueneza injili lakini vilevile kutafuta kilichopotea hivyo viongozi wa dini wanaisaidia Serikali hususani watu walioshindikana.
Lengo la kongamano hilo ni kuleta chachu au kuchochea uinjilishaji, kuibua viongozi wa dini na masuala ya miradi ya maendeleo inayogusa jamii, kongamano ambalo limehudhuriwa na viongozi wa mbalimbali Maaskofu na Wachungaji wa TAG, Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
RC amesema pia viongozinwa dini wanauwezo wa kubadili tabia ovu iliyoko kwa jamii hatimaye kuwa na jamii yenye maadili mema. ” Lazima tuamini watu wanaopewa maono ambayo yana masilahi mapana ya watu ” amesema RC Chalamila.
Aidha RC Chalamila ametoa rai kwa viongozi wa Dini wote walioshiriki katika Kongamano hilo kutambua kuwa wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa wale wanao waongoza ambao ndio wafuasi wao, pia amewataka kwenda kujenga jamii yenye mawazo chanya hususani vijana kuhusu ajira amesistiza vijana lazima wajiamini na wajipambanue kutafuta fursa za kujipatia kipato mara wanapo maliza masomo na sio kusubiri kuajiriwa na Serikali.
Kwa upande wa Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Mtokambali ametoa Shukrani kwa Mungu kwa kuwa na kiongozi wa Serikali Mhe Albert Chalamila katika Kongamano hilo ambaye ni mwakilishi wa Rais katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema Dira ya Uamusho ya miaka 13 ya TAG ina mambo makuu matati la kwanza kueneza injili, pili kuibua viongozi na tatu suala la miradi ya maendeleo kwa jamii .
“Kwa sababu uwezi kuwa na jamii iliyogubikwa na wimbi la umasikini hivyo kongamano hilo lilianza rasmi Jumatatu linatarajia kuhitimishwa Ijumaa Septemba 15, 2023 ambapo katika kipindi chote cha kongamano kusudio kubwa ni kukumbushana na kupeana chachu au kuchochea namna bora ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kama viongozi wa kiroho.
Mwisho Baba Askofu ametoa ombi maalum kwa Serikali kupitia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kujenga ikumbi mkubwa wa mikutano, pia mwaka ujao 2024 TAG inatimiza miaka 85 kilele cha Seherehe hizo kimependekezwa kufanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Vilevile kwa namna ya pekee amemkabidhi RC Chalamila zawadi ya Biblia ambayo itamsaidia kumuongoza katika utekelezaji wa majukumu yake ya kiutumishi wa umma.