Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani katika viwanja vya Zakhiem Mbagala Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amekemea tabia za kutozingatia taratibu za usafi kama vile kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi na hata madereva wa bodaboda wanavyopaki ovyo barabarani amesema kituo chochote kikiwa mahali pasipo sahihi ni uchafu hivyo usafi ni pamoja na mtu kuwa katika eneo lake stahiki.
Aidha Chalamila amesema suala la usafi na Usalama wa Mkoa ni ajenda za kudumu katika Mkoa” Taka ni Uchafu na Uchafu ni maradhi, tengenezeni By Laws za kudhibiti uchafu na jamii lazima itii sheria bila shuruti ” amesema.