Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema suala la kulipa kodi ni lazima kwani inasaidia nchi kutengeneza na kuboresha miradi mbalimbali yenye kuleta maendeleo kwa taifa.
Chalamila amesema hayo jana, jana wakati wa utoaji wa Tuzo kwa walipa kodi waliofanya vizuri mikoa yote ya kikodi kwa mwaka 2024/2025.
“Kila mtu nchini alipe Kodi kwa kiasi chake na kinachostahili bila kuangalia kuwa huyu ni tajiri au masikini bali watoke kulingana na kiapato chao.Pesa inayopatikana kupitia makusanyo inaonekana wazi hasa katika mkoa wa Dar es salaam kwani ujenzi wa barabara katika maeneo ya mji unaendelea tena kwa kasi hivyo huo ni ushahidi tosha,”Amesema Chalamila.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-19-1024x683.png)
Ameongeza,”ujenzi wa reli na treni ya kisasa imetokana na kodi hizo na kizuri zaidi hivi karibuni mkataba mwingine wa ujenzi wa reli kutoka Uvinza mpaka Burundi ambao utagharimu zaidi ya bilioni tano tayari umekwisha sainiwa,”
Chalamila amemtaka Kamishna Mkuu wa TRA, kuendelea kutoa elimu kwa kuanzisha utamaduni wa kulipa kodi ili ikitokea mmoja wa walipa kodi amepatwa na changamoto au ameanguka kimtaji wawepo wengine wakuendelea kodi ili nchi iweze kujisimamia na kuondoa utegemezi.
Amesema ni muhimu kila mtu kutoa risiti unapouza chochote na unaponunua dai risiti ilikuepuka ukwepaji kodi na kufanya jamii iwe nautamaduni wa kulipa kodi kwa hiari.Pia amesema katika kuelekea ufanyaji wa biashara masaa 24 ushirikiano wa TRA ni muhimu kwani itasaidia kukusanya kodi na kuongeza pato la Taifa.
“Katika kufanya biashara masaa 24 ni wazi mfanyakazi wa TRA kutokulala bali kukesha kwani ulinzi umeimalishwa na ndio muda wa kuondoa upungufu wa ajira kwa vijana sababu wataweka biashara zao maeoneo yote nanyi mtakusanya kodi,”amesema Chalamila.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-20.png)
Aidha, Chalamila amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumchangua Yusuph Mwenda kuwa Kamishna Mkuu kwani alipewa Mamlaka ikiwa kwenye changamoto lakini ameweza kuimalisha uongozi ndani ya Mamlaka hiyo na kuondoa manung’uniko yote.
Naye Kamishina Mkuu wa (TRA) Yusuph Mwenda amesema Mamlaka hiyo itaendelea kusimamia usawa katika kulipa kodi ili kila mtu alipe kinachostahili.
Mwenda amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kutoa miongozo ya utekelezaji wa majukumu na kuisimamia kwani mafanikio ya mkoa wa dar es salaam yananchango mkubwa kutoka kwake.
“Mapato hayo ambayo Mamlaka imekusanya si yamechangiwa na Rais Samia bali na Mkuu wa mkoa kwani umekuwa si msimamizi bali mkusanya Kodi,dar es salaam si mkoa tu bali ni jiji la kibiashara na kwa kipindi kifupi TRA imefanikiwa kukusanya trioni 16.5 na kati ya fedha hizo trioni 13 zimetoka jiji la kibiashara sawa na asilimia 85 ya nchi nzima,”amesema Mwenda .
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-21-1024x683.png)
Ameongeza,”tutaimarisha mifumo yote ya kibiashara ili kuleta utulivu kwa Wafanyabiashara iliwafanye biashara zao vizuri na kurahisisha kulipa kodi,”
Na kuongeza kuwa mafanikio hayo makubwa nikutokana na uwepo wa vituo vya forodha, ukusanyaji wa Kodi za mafuta pamoja na uwanja wa taifa.
Mwenda amesema Mkoa wa Dar es salaam unawafanyabiashara zaidi ya milioni 3 waliogawanyika katika makundi mawili ambayo ni wafanyabiashara na wale walioajiriwa hivyo ilikuendelea kukuza pato la nchi ni lazima kila mtu ajisajili ilikulipa kodi kwa hiari kusimamia usawa.
Amesema TRA itaendelea kupambana na wanaojihusisha na magendo kwa kuimarisha ulinzi maeneo kama mbweni na Kunduchi kwani wapo watu wachache wenye nia hovu hivyo tutaendelea kuwashughulikia.
Mwenda amewataka walipakodi kuendelea kufanya vizuri ili mwakani wapokee tuzo zenye jina la Rais Samia Suluhu Hassan kama alivyoagiza.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-22-1024x683.png)
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-23-1024x683.png)