RNa Mwandishi Wetu,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Octoba 1, 2023 amefika eneo la ajali ya moto Kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo moto umetokea majira ya asubuhi na kusababisha kuteketea jengo moja pamoja na baadhi ya bidhaa zilizokuwemo katika jengo hilo.
RC Chalamila akitoa taarifa ya Serikali kufuatia janga hilo amesema hadi saa 4:15 asubuhi taarifa aliyo nayo hakuna mtu aliyepoteza maisha au majeruhi kufuatia janga hilo, ametoa pongezi kwa vyombo vya ulinzi na usalama hususani Jeshi la Zima Moto kwa kuzidhibiti moto huo usisambae lakini pia Jeshi la Polisi kuhakikisha hakuna wizi au upotevu wa mali za wafanyabishara.
Aidha RC Chalamila amewataka wananchi kuendelea kuchukua taadhari dhidi ya majanga ya moto wakati wote pia amekemea kitendo cha kiziba vipenyo au njia kati ya jengo moja na jingine ambayo husababisha majanga ya moto yanapotokea magari ya zima moto hushindwa kupita hivyo waliojenga kuzuia vinjia hivyo kwa mujibu wa ramani ya mipango miji kuvunja mara moja
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka wafanyabishara wa Kariakoo na Wananchi kwa ujumla kuwa watulivu, ambapo amelipongeza Jeshi la zima moto, Polisi na wadau wengine kama DAWASA kwa kushiriki kikamilifu kuzuia kusambaa kwa moto huo ambao ungeweza kuleta madhara makubwa zaidi.