Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Holmes Matinyi kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan

Hafla ya uapisho huo imefanyika leo Julai 4, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkoa huo Ilala Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vongozi mbalimbali wa Sekretarieti na Wilaya za mkoa huo wakiongozwa na katibu Tawala wa Mkoa Rehema Madenge.

RC Chalamila amemtakia majukumu mema katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Temeke huku akitoa rai kwa Viongozi wa Manispaa na Wilaya kumpa ushirikiano kiongozi huyo.