Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Septemba 15, 2023 amekutana na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Dk Jabiri Bakari alipozuru Ofisi za mamlaka hiyo eneo la Mawasiliano Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamiana lakini pia kwa sababu ya umuhimu wa mamlaka hiyo ambayo ni Mamlaka dhibiti ya Mawasiliano hapa nchini.
RC Chalamila amesema mamlaka hiyo ina mchango mkubwa katika mambo kadhaa na ndio maana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa sana katika Teknolojia ya Kisasa, Rasilimali watu na vifaa vya kisasa ili kuwezesha mamlaka hiyo kukabiliana na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yanayoikabikabili Dunia.
Aidha Chalamila amesema teknolojia inavyokua ina changamoto zake na ndio maana unaweza usione bunduki mahali popote lakini kutoka na kukua kwa teknolojia bado nchi ikaingia katika machafuko hivyo mamlaka hii ni muhimu katika Kuimarisha usalama wa nchi.
Kwa kutambua umuhimu huo Ofisi yake pamoja na Kamati ya usalama ya mkoa imepanga kufanya ziara katika mamlaka ya ya mawasiliano kwa lengo la kujifunza ili kukabiliana na athari za madiliko ya makuzi makubwa ya Teknolojia.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt Jabiri Bakari amesema mamlaka imejipanga vizuri kukabiliana na mabadiliko makubwa ya kiteknolojia bila kuathiri makuzi ya kiuchumi katika Taifa