Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akagua miradi mbalimbali inayoendelea katika jiji la Dar es Salaam.
Chalamila akagua miradi hiyo ikiwa ni moja ya maandalizi ya mkutano mkuu wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati.
Mkuu wa Mkoa amekagua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu wa Mwalimu Julius Nyerere alipotembelea eneo la terminal 1.
Aidha RC amekagua barabara ya Nyerere ambapo ameagiza kufungwa kwa taa za barabarani ifikapo Januari 20.
Mkuu wa mkoa ameagiza kuwa magari makubwa aina ya (malori) kuacha kupaki katika maeneo ya barabara (road reserve) na kuagiza wamiliki wa malori kutafuta eneo la kupaki magari hayo.
Mkuu wa mkoa ameeleza kuwa Watanzania watanufaika na ugeni huo kwa kuruhusiwa kufanya biashara masaa 24.
Mkuu wa mkoa amewaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kudumisha usafi kwa kuweka mazingira safi katika maeneo yotee.Katika ziara yake Mkuu wa Mkoa ameagiza kufungwa kwa barabara ya stesheni kuelekea Johari Rotana kwa watumiaji wa pikipiki na bajaji ifikapo tarehe 20.