Ratiba ya mazishi ya mama yetu mpendwa Peres Kingunge Ngombale Mwiru(Mama Kinje) Jumatano tarehe 10/1/2018- Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street.-Saa 11:00 jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha) ****************************** Alhamisi tarehe 11/1/2018-Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.-Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote-Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana kuaga mwili wa marehemu(waombolezaji wote)-Saa 7:15 mchana mwili kuelekea kanisa la St. Peter’s Oysterbay Kwa ibada(waombolezaji wote)-Saa 7:30 mchana -8:30 mchana ibada ya kumuombea marehemu-Saa 8:30 mchana mpaka 9:30 mchana kuaga mwili wa marehemu Kanisani.-Saa 9:45 mwili kuelekea makaburini Kinondoni.-Saa 10:00 jioni 12:00 jioni shughuli za mazishi( waombolezaji wote)-Saa 12:00 – waombolezaji wote kuelekea nyumbani Kwa Mzee Kingunge victoria.-Saa 1:00 usiku – saa 2:30 usiku kupata chakula cha jioni Kwa waombolezaji wote.
Tunawashukuru sana Kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu Mungu awazidishie sana. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Omary A. Kimbau( msemaji wa familia)