Wapatanishi wa mzozo wa Israel na Hamas, ambao ni Marekani, Qatar na Misri wametoa rasimu ya mwisho ya makubaliano ya kuvimaliza vita huko Gaza leo Jumatatu. Hayo yamesemwa na maafisa kwa shirika la habari la Reuters.
Mazungumzo hayo yaliozusha mjadala wa muda marefu yalifanyika usiku wa kuamkia leo na kulihudhuriwa na mjumbe wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump.
Afisa huyo alisema mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka yamefanyika mjini Doha, Qatar yakimuhusisha mkuu wa shirika la ujasusi la Israel (Mossad) David Barnea, mashirika ya kijasusi ya Shin Bet na maafisa kutoka Marekani.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa saa 24 zijazo zitakuwa muhimu katika kufikiwa kwa makubaliano hayo.
Hata hivyo, Mataifa hayo wapatanishi yamefanya kazi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja kwenye mazungumzo ya kumaliza vita huko Gaza bila mafanikio.