Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio anatarajiwa kuwasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ili kushiriki Mkutano wa Nchi za Afrika unaohusu Nishati.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Kombo katika mkutano wake na Waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais Bio atakuwa Rais wa kwanza kuwasili kati ya wengine watakaowasili kesho na kesho kutwa kabla ya Mkutano huo utakaoanza Januari 27 na 28 mwaka huu.