Rais wa kwanza wa Namibia huru, Sam Nujoma, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 katika mji mkuu wa Windhoek, kiongozi wa sasa wa nchi hiyo ametangaza.

Nujoma aliongoza vita vya muda mrefu vya kudai uhuru kutoka kwa Afrika Kusini mwaka 1990 baada ya kusaidia kupatikana kwa vuguvugu la ukombozi la Namibia lililojulikana kama South West Peoples’ Organization (Swapo) miaka ya 1960.

Baada ya uhuru, Nujoma alikua rais mwaka 1990 na aliongoza nchi hadi 2005.

Nujoma alikuwa amelazwa hospitalini kwa muda wa wiki tatu zilizopita kutokana na ugonjwa ambao “hakuweza kupona”, Rais wa Namibia Nangolo Mbumba alisema katika taarifa yake akitangaza kifo hicho kwa “huzuni na masikitiko makubwa”.

Aliongeza: “Baba yetu mwanzilishi aliishi maisha marefu na yenye matokeo ambayo alitumikia kipekee watu wa nchi yake anayoipenda.”

Nujoma alistaafu kama mkuu wa nchi mwaka 2005, lakini aliendelea kukiongoza chama hicho kabla ya kung’atuka mwaka 2007 kama rais wa chama tawala cha Swapo baada ya kukiongoza kwa miaka 47.