RAIS wa Korea Kusini aliyeachishwa kazi Yoon Suk Yeol amekamatwa, kulingana na mamlaka, na kuweka kihistoria nchini humo.
Yoon ambaye anachunguzwa kwa uasi ndiye rais wa kwanza aliye madarakani nchini humo kukamatwa.
Baadhi ya wachunguzi waliingia katika makazi ya Yoon kwa kutumia ngazi
Wachunguzi waliingia katika makazi ya rais kwa kutumia ngazi, Yonhap inaripoti.
Walizuiliwa mapema na wabunge wa chama tawala na mawakili wa Yoon kwenye lango la kuingilia, pamoja na kizuizi cha magari kilichowekwa.
Lakini baadhi ya wachunguzi waliripotiwa kufanikiwa kufikia eneo hilo kupitia njia iliyo karibu ya kupanda mlima.
Na hivyo ndivyo wachunguzi hao walivyofanikiwa kuingia nyumbani kwa rais, mamlaka imethibitisha.
Waandamanaji wamekuwa wakionekana mara kwa mara wakikita kambi katika makazi yake katika kipindi cha wiki chache zilizopita na asubuhi hii umati mkubwa wa watu ulijitokeza tena – wakitazama jinsi wachunguzi wanavyoendelea katika jaribio lao la pili la kumkamata Yoon.