Baada ya siku ya maandamano, ghasia na umwagaji damu, Rais wa Kenya William Ruto alihutubia taifa kwa ujumbe wa huzuni na wenye nguvu.
Akisema maandamano “halali” dhidi ya sera zake “yametekwa nyara na kundi la wahalifu waliopangwa,” alionya serikali yake itatumia njia zote ili kuzuia kujirudia kwa ghasia hizo, “kwa gharama yoyote”.
“Matukio ya leo yanaashiria hatua muhimu ya jinsi tunavyokabiliana na vitisho vya amani yetu,” alisema. “Tutahakikisha hali ya aina hii haijirudii tena.”
Ujumbe wa rais ulikuwa jaribio la kunyakua udhibiti baada ya siku kadhaa za maandamano ya mitaani ambayo yameongezeka kwa nguvu. Siku ya Jumanne, waliongezeka huku watu wasiopungua watano wakipigwa risasi na mamia kujeruhiwa.
Lakini kwa muda mrefu baadhi ya watu wa Bw. Ruto lazima wahofu kwamba huenda mambo yasiwe rahisi sana, na kwamba bado kuna hatua ngumu za kuchukua siku za usoni.
Alipochaguliwa mwaka wa 2022 aliahidi kupunguza ufisadi, kuinua uchumi wa nchi unaodorora na kusaidia maskini, Lakini Bw Ruto sasa anakabiliwa na uasi usio na kifani dhidi ya muswada anaosema kuwa ni sehemu muhimu ya mpango wake wa kujenga taifa.
Huenda ikawa rahisi kujua ni hatua gani angechukua iwapo upinzani anaokabiliana nao Bw.Ruto ungesalia ndani ya bunge.