Rais, 72, alianguka alipokuwa akipanda ngazi kwenye gari ambalo lilipaswa kumpeleka karibu na Bustani ya Eagle Square katika mji mkuu, Abuja. Ilibidi asaidiwe kusimama. Mmoja wa wasaidizi wake alielezea kama “hatua mbaya” na akasema rais ameweza kuendelea na programu iliyobaki.
“Mara moja aliendelea na sherehe hiyo. Hakuna masuala,” aliandika msaidizi wa rais Dada Olusegun kwenye X. Mpinzani wa karibu wa Bw Tinubu wakati wa uchaguzi wa mwaka jana, Atiku Abubakar, alionyesha huruma yake.
“Ninamuhurumia kwa dhati Rais Bola Tinubu kuhusu tukio hili lisilo la kufurahisha alipokuwa amepangwa kukagua gwaride la Siku ya Demokrasia. Ninatumai kuwa kila kitu kiko sawa naye, “aliandika kwenye X.
Mwanasiasa maarufu na mwanaharakati Shehu Sani alisema haikuwa jambo kubwa, na kwamba tukio hilo lilionyesha rais hana tofauti na mtu mwingine yeyote.“Si Rais Tinubu pekee, yeyote aliye hai anaweza kujikwaa na kuanguka; ilitokea kwa Rais Biden na Fidel Castro. Marais ni binadamu.
”Mtumiaji wa X Arinze Odira alisema kuanguka “kunatisha kutazama”.Mnigeria mwingine Charles Awuzie alichapisha kwenye Facebook kwamba alipata hisia baada ya kuona klipu hiyo.”Iwapo ni Rais Biden au Rais Tinubu, kwa kawaida mimi huhisi uchungu wakati mwanadamu anajeruhiwa mahali pa huduma.
Namtakia heri rais.”Wakati Wanigeria wengi wameonyesha huruma na kumtakia heri, kwa baadhi imezua maswali mengi kuhusu afya yake, ambayo ilihojiwa na wapinzani wake wakati wa kampeni za uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali mwaka jana.