Na Mwandishi Wetu, JammhuriMedia, Songea
RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema mafanikio yaliyopo sekta ya kilimo hayatokei kwa bahati mbaya bali ni kutokana na juhudi z kubwa zilizofaywa na Serikali.
Amesema zao la kahawa pekee limeongezeka katika uzalishaji kutoka tani 65 hadi kufikia tani 85,hivyo kuingiza dola milioni 250 nchini.
Ameitaka Wizara ya Kilimo kuhakikisha wawekezaji waliopo mbali wanayoyafanya katika kurudisha kwa jamii za wanahusisha kurithisha ujuzi na teknolojia hususami za Umwagiliaji zinazotumika katika sekta hiyo ili kuwezesha wananchi kuwa na kilimo chenye tija kwa maslahi ya vizazi vijavyo.
Rais Samia amesema hayo alipotembelea shamba la uzalishaji wa Kahawa la AVIV mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maghala 28 ya kuhifadhi mazao ya nafaka yaliyo chini ya Wakala wa hifadhi ya Chakula (NFRA) wilayani Songea mkoani Ruvuma katika muendelezo wa ziara yake ya siku sita mkoani huko.
Amesema, matokeo makubwa na mafanikio yaliyopo sekta ya kilimo si bahati mbaya bali unatokana na juhudi za serikali
Rais Samia ametaka wakulima watumie fursa ya kupanda kwa bei ya kahawa, kuhifadhi fedha ili wasitaabike kipindi bei itakapo shuka.
“Misimu ikiwa mizuri na bei ikiwa nzuri tuwe na mifumo ya kujiwekea akiba ili mabadiliko ya tabianchi yanapotokea tuwe na Akiba,” amesema.
Ameitaka Wizara ya Kilimo kujipanga vyema na masharti yanayotolewa na masoko ya kimataifa ya kahawa hasa lile la uzalishaji bila kukata misitu.
Pamoja na kutokata misitu, amesema masharti mengine ni kukagua, kuyasajili na kupeleka taarifa za mashamba kwenye masoko hayo ili ijulikane linakotoka zao husika.
“Wanatambua tusikate misitu,kule kwao wameshakata lakini sisi tunataka soko, tunapaswa kuhakikisha tunayatimiza masharti ili kupata soko,” amesema.
Pia ameagiza wizara kufanya uchunguzi wa madai ya wakulima wa kahawa kukatwa fedha kinyemela na vyama vikuu vya ushirika.
Amesema anatambua kuwepo kwa malalamiko hayo yaliyosababishwa na ongezeko la bei ya kahawa mwaka huu.
“Nnatambua uwepo wa malalamiko ya wananchi kwamba kwa sababu kahawa imepanda bei baadhi ya vyama vikuu vya ushirika (hakuvitaja) vinawakata wakulima kinyemela,” amesema.
Amemtaka Waziri Bashe afuatilie ili kuwa na mfumo wa wazi utakaowafanya wakulima kuona wanachouza na uhalisia wa makato Yao.
“Huu ujanja ujanja unaoendelea unapaswa kukomeshwa,” amesema Mkuu huyo wa nchi alipotembelea shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 200.
Hata hivyo, amesema ongezeko la bei hiyo na malipo ya haraka kwa wakulima wa kahawa ni matokeo ya juhudi za Serikali za kuongeza ufanisi katika mauzo ya zao hilo.
Katika hatua nyingine, Rais Samia ameutaka uongozi wa shamba hilo,kufanya shughuli za kijamii,ujikite katika uchimbaji wa visima vya umwagiliaji kwenye mashamba ya wakulima.
Amesema kufanya hivyo, kutawawezesha wakulima kuzalisha kahawa kwa umwagiliaji na kuuza kwa Aviv.
Awali, akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Bashe amesema shamba hilo ni moja kati ya 50 yanayozalisha kahawa na kwamba hilo ni kubwa zaidi ya mengine yote.
Amesema asilimia 60 ya kahawa inayozalishwa na shamba hilo inauzwa nje ya nchi kwa Kampuni ya Strabag.
Hata hivyo, amesema wastani wa bei ya kahawa mwaka huu ni Dola 4.3 za Marekani, kiwango ambacho ni tofauti na nyakati zilizopita.
Kwa upande wake,Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe(Mb), amesema mafanikio yaliyopo sekta ya kilimo yametokana na maamuzi ya kisera na sheria ya Rais Dkt. Samia hususani katika kuboresha sekta ya uwekezaji na kurudisha masoko.
“Hali hii imerudisha uhai wa uzalishaji kwa wawekezaji na wakulima wa ndani,shamba hili linategemea zaidi shughuli za umwagiliaji hivyo Wizara tumemuagiza muwekezaji uchimbaji wa visima na mabwawa unufaishe jamii katika mashamba ya wananchi,”amesema.
Amesisitiza kuwa shamba la AVIV Tanzania Ltd ni moja kati ya mashamba 50 makubwa yanayozalisha kahawa nchini, likiwa na zaidi ya hekta 2,000, ambapo zaidi ya hekta 1,000 zimeshapandwa kahawa. Uzalishaji wa kahawa umeongezeka kutoka tani 60 hadi kufikia tani 85 na kwamba shamba hilopia limeanza kuotesha pilipili manga (black pepper) na kuuza nje ya nchi, likiwa na uzalishaji wa tani 2 na lengo la kufikia tani 3.
Ameongeza kuwa ujenzi wa maghala 28 yenye gharama ya shlilingi bilioni 14.7 Sawa na sh bilioni 527 na uwezo wa kuchukua tanı 1,000 kwa kila moja yanajengwa na serikali mkoani humo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama, ameishukuru serikali kwa maamuzi ya kisera yanayovutia uwekezaji na kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali. Ameeleza kuwa mradi wa AVIV umekuwa na faida nyingi kwa jamii, na mwekezaji ameshirikiana na uongozi wa serikali kuandaa mpango wa urithishaji wa mchakato wa kilimo cha kahawa. Mwekezaji huyo pia anachangia hadi bilioni 1 kwa halmashauri ya Peramiho