Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

WAZIRI wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Damas Ndumbaro ametembelea na kukagua mabanda ya maonesho ya Tamasha la Tatu la Utamaduni kitaifa ambalo kilele chake ni Septemba 23, mwaka huu, huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.

Dkt.Ndumbaro akiwa kwenye banda la benki ya NMB tawi la Songea na aliongea na meneja wa benki hiyo Olipa Hebet alisema kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa inaboresha huduma mbalimbali za maendeleo kwa wananchi ambao wanahitaji kupata huduma za kibenki, mikopo kiwemo ya kilimo na biashara.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damasi Ndumbaro alipotembelea Banda la NMB kulipa ni meneja wa Benk hiyo Olipa Hebet

Aliishauri benki hiyo kuona umuhimu wa kuendeleza Kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na wananchi ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu ya ujasiriamali jambo ambalo itapelekea kutumia vizuri fedha wanazokopeshwa baada ya kupata mikopo.

Waziri Dkt.Ndumbaro akiwa kwenye banda la Wizara ya Ardhi aliwahimiza wataalamu wa idara hiyo kuona umuhimu wa kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa wakikabiliwa na migogoro mbalimbali ya ardhi kwenye maeneo yao na kupelekea kuleta migongano ya wenyewe kwa wenyewe.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo akisaini kitabu Cha wageni katika Banda la Ardhi kulia ni Kamisha said Juma Kijiji.

“Kumekuwa na migogoro mingi inayohusu ardhi na hata viwanja katika maeneo mbalimbali nchini hivyo ni jukumu la wizara ya ardhi kushughulikia migogoro hiyo kwa ukaribu ili kuipatia ufumbuzi ambao utapelekea kuwepo kwa amani miongoni kwa jamii”alisema.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Songea Said Juma Kijuji alisema kuwa Wizara ya Ardhi kupitia ofisi yake imekuwa ikisikiliza kero mbalimbali za migogoro ya ardhi hivyo imefunguliwa kliniki ya kusikiliza na kutatua kero zinazoletwa na wananchi kuhusiana na migogoro hiyo jambo ambalo limekuwa ni jawabu kubwa kwa wananchi.

Kijuji amewashauri wananchi kuitumia kliniki hiyo sambamba na kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima kwenye maeneo yao kwani kuwepo kwa migogoro hiyo mara nyingi imepelekea kurudisha nyuma jitihada za wananchi za kujiletea maendeleo na kwamba pale inapojitokeza migogoro ni vyema wao kwenye maeneo yao wakaanza kukaa na kuitatua kabla ya kufikishana mbali.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo akitoa maelezo kwenye banda la TRA Mkoa wa Ruvuma.
          
Please follow and like us:
Pin Share