Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia
Dar es Salaam

Kanisa la Africa Inland Church Tanzania AICT Pastorate ya Magomeni Dayosisi ya Pwani Washirika wa mwili wa Kristo wanayo furaha kusherekea ibada ya kumrudishia Mungu shukrani,heshima,sifa na utukufu, Oktoba 27, 2024 Jublee ya miaka 50 tangu kuanzishwa kanisa hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 17, 2024 Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Pwani Philipi Mafuja amesema katika ibada hiyo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na tayari amethibitisha kujumuika nao kwenye misa hiyo maalum ya kumtukuza, kumsifu, kumuabudu na kumuomba katika kuelekea kuadhimisha Jubilee ya miaka 50 (Golden Jubilee) ya Kanisa la AICT Pastoreti ya Magomeni tangu kuanzishwa na kutoa huduma ya Blbwana .

“Kuelekea siku hiyo tutakuwa na sgughuli zingine za kiroho na kijamii ikiwemo tamasha la uimbaji,maombi, matendo ya huruma na upendo kwa jamii inayotunzunguka kwa kugawa mitungi ya gesi kuunga mkono juhudi za Mhe Rais katika agenda ya nishati safi na kutembelea vituo vya watoto yatima kuwajulia hali na kushirikiana nao” amesema Askofu Philipo

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuwataarufu mamilioni ya waumini kujumuika katika shughuli hii itakayofanyika hapo Kanisa la AICT Pastoreti ya Magomeni ambayo itakwenda sambamba na na harambee ya kukamilisha ujenzi wa Kanisa unaondelea ili ukamilike .

Aidha amewashukuru Watanzania wa dini na medhehebu yote ambao wamepokea kadi za michango ya sadaka ya ujenzi na wametoa ahadi wengine wameshachangia tayari Bwana awabariki sana kwani sote tunamwabudu Mungu mmoja alituumba kwa mfano wa sura yake.

Please follow and like us:
Pin Share