Na Tiganya Vincent , JamhuriMedia, Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuongeza jopo jingine la Majaji wa Mahakama ya Rufaa ili kuendelea kupunguza mrundikano wa mashauri mashauri.
Ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Mei 2023 wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Majaji 6 wa Mahakama ya Rufani iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma kufuatia uteuzi aliufanya hivi karibuni.
Dkt.Samia alisema lengo ni kufikisha Majopo ya Majaji wa Mahakama ya Rufani 10 badala ya tisa(9),hatua hiyo itasaidia kuharikisha utoaji haki kwa wananchi kwa mashauri ya Rufani.
“Nawapenda kukupongeze Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kupata Jopo jipya la Majaji wa Mahaka ya Rufaa na kila nitakapokuwa nikiteua nitaongeza idadi ya wanawake ili kufikia wastani wa hamsini kwa Hamsini kwa Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufaa”amesisitiza.
Ameongeza kuwa sanjari ya kuongeza Jopo ya Majaji wa Mahakama ya Rufani pia ataongeza Majaji wa Mahakama Kuu wapya kwa lengo la kuhakikisha utoaji wa haki kwa wananchi unafanyika kwa wakati.
Naye Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema uteuzi na uapisho alioufanya Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan uweka historia kwa ongezeko la idadi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Amesema kuwa kabla ya Rais Samia kuingia madarakani , Majaji wa Rufani walikuwa hazidi 16 na alipoingia aliongeza na kufikia 25 na uapisho mpaya umefanya wafikie Majaji wa 31 hapa nchini.
Mhe. Prof. Juma alisema hatua hiyo umesaidia Mahakama ya Rufaa kuongeza Majopo ya Majaji wa Rufani kutoka 7 hadi kufikisha Majopo 9 ambapo kwa wastani kila Jopo ni Majaji 3, 5 hadi 7.
Amesema faidia ambayo Mahakama imeipata kutokana na uteuzi huo ni kupungua kwa mzigo wa mashauri ambao kila jopo lilikuwa likiubeba amabpo kwa wastani yalikuwa mashauri 805 na sasa yatafiki 626.
Aidha Jaji Mkuu huyo wa Tanzania aliwataka Majaji kubadili mtazamo ikiwemo kuangalia matumizi ya usuluhushi kwa baadhi ya mashauri ikiwemo ya biashara ili kupunguza mrundiko wa mashauri ambayo yangeweza kumalizika kwa mazungumzo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson aliitaka Mahakama ya Tanzania kupeleka mapendekezo ya maeneo ambayo ni kikwazo katika utoaji wa haki ili Bunge lifanyie marekebisho Sheria na hatimaye wananchi wapate haki kwa wakati bila kucheleweshwa wala kufunikwa.