Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wakati akiwa njiani kuelekea Mkoani Dodoma tarehe 18 Julai, 2024.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Songwe Ndugu Daniel Chongolo wakati alipowasili Tunduma mkoani Songwe akitokea Sumbawanga mkoani Rukwa alilofanya ziara ya kikazi ya siku tatu akizindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Shule ya Msingi Tunduma, Ebenezer Wile Mwakasyele (8) ambaye ni mlemavu akiwa pembezoni mwa barabara wakati akimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia wananchi Tunduma Mkoani Songwe tarehe 18 Julai, 2024. Mhe. Rais Dkt. Samia ametoa maagizo kwa Ofisi yake pamoja na Wizara ya Afya kuhakikisha Mtoto huyo anatengenezewa mguu wa bandia mara moja.