Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Chama cha Mawakili wa Serikali, Nembo ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mfumo Rasmi wa Ofisi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali Jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujionea shughuli mbalimbali pamoja na huduma zitolewazo na Ofisi hizo kabla ya kuhutubia na kuzindua Rasmi Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kwenye laptop kuzindua mfumo rasmi wa Kieletroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAGMIS), nembo ya Ofisi hiyo pamoja na Chama cha Mawakili wa Serikali katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022.
Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022.