Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025. Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Angola Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço na lengo la Ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano ya kihistoria na kidugu baina ya Tanzania na Angola.