Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Namtumbo

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwahimiza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa,wenyeviti wa vitongoji ,wenyeviti wa vijiji na kamati zao wakachague wale wenye sifa na wale wenye sifa ya kugombea wakagombee bila kutiana mizwengwe wala fitina.

Rais Samia ameyasema hayo leo wilayani Namtumbo wakati akizungumza na wanachi wa vijiji, Litola , Rwinga na Mchomoro ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani Ruvuma ya kutembelea,kukagua, na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Kata ya Litola, Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma tarehe 26 Septemba, 2024.

“Wengine wanaenda kuchaguwa wengine hawaendi baadae akishapatika kiongozi wamaanza kulalamika kiongozi Gani mmbovu hana uwezo lakini kama mngeenda kumchagua mangempata kiongozi anayemtaka hiyo tutoke tukachague viongozi wetu.

“Mmeona mwelekeo wa serikali yetu ni maendeleo ya kwenda mbele ,kwenye maji kwenye kilimo, kwenye umeme kwa hiyo nendeni kajipangeni vizuri mkachague viongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi ili maendeleo yawe juu.

“Tarehe 20 mwezi hujao ni kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura na hii ni tofauti na kuboresha daftari la wapiga kura nchini kwa hiyo madiwani, wakuu wa wilayani wahimize wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuhakikiwa” amesema Rais Samia.

Hata hivyo alihimiza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa kwa umoja na uwazi. Alisisitiza umuhimu wa uchaguzi wa haki katika kukuza maendeleo ya jamii.

Samia alifafanua kwamba viongozi bora watasaidia kuleta mabadiliko chanya, huku akiwataka vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi katika mchakato huo. “Chagueni viongozi wanaowakilisha maslahi yenu,” alisema, akiwataka wananchi kuimarisha demokrasia na ushirikiano katika maendeleo yao.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa amemshukuru Rais Samia kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo amejenga zahanati 13 mpya , wameboresha hospital yao ya wilaya , wamepokea vifaa tiba vyenye thamani ya sh. Bilioni 2.5 , ambapo 2021 kulikuwa na changamoto ya dawa lakini leo walivyoingia dawa zinafika kila wakati.

Alisema upande wa elimu anaamini ukitaka kumfikia mwananchi wa kawaida muelimishe mtoto wake na rais ameweza kufanya hivyo ameweza kutoa kiasi cha sh. Bilioni 13 kwa ajili ya kujenga shule, madarasa mapya 207,shule mpya nne,tumejenga shule mpya tatu za shule ya msingi kuanzia chekechea mpaka darasa la saba,umetuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya Chuo Cha VETA ya kisasa kiasi cha sh. Milioni 553, maji tumepokea kiasi cha sh. Bilioni 17.2 umeokoa akina mama ambao walikuwa wapoteze maisha yao kwa ajili ya kwenda umbali mrefu kutafuta maji.

Na miradi ya bilioni 9 ya maji inaendelea katika jimbo hilo kwa hiyo umemtua mama ndoo kichwani kwa kuwaletea maji.

“Namtumbo mji unaongezeka kuna taasisi hapa, kuna ofisi za Serikali na watu binfasi, wafanyabiashara wakubwa na wadogo tunaomba Rais kiasi cha sh bilioni 6 kwa ajili ya kupongeza mradi mwingine wa maji , Wizara haina hela mama wewe ndio mwenye hela tunaomba fungua pochi utupatie fedha.

Wananchi wa Kata ya Litola Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, waliojitokeza kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 26 Septemba,2024

“Hata kama unabahati kiasi Gani huwezi kuokota nyumba nyumba inajengwa leo hii watoto wanaenda shule watoto wanaenda maliwato mazuri na hapa umetujengea shule kubwa kabisa na nzuri kesho tunakukaribisha uje uione.

“Sisi tunashida kubwa ya Tembo kaya mia nne wameathirika na tunaomba juhudi zichukuliwe kuzuia hawa Ndovu” amesema.

Please follow and like us:
Pin Share