Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfried Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mhe. Hamis Mohamed Mwinjuma kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Dkt. James Henry Kilabuko kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Mhe. Dkt. Stephen Justice Nindi, kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo (anayeshughulikia masuala ya Ushirika na Umwagiliaji), kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha mabalozi wafatao;
▶️Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa.
▶️Bw. Mobhare Holmes Matinyi.
▶️CP Hamad Khamis Hamad.
▶️CP Suzan Salome Kaganda
▶️Bw.Thobias Masandiko Makoba, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024.