Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Samia suluhu Hassan, amesema Utekekezaji wa Dira ya Mwaka 2020/2025 ina mabadiliko makubwa ikiwemo katika Sekta ya utoaji haki ambapo jumla ya Mashauri 271 yalisajiliwa kupitia mtandao huku mashahidi waliopo nje ya nchi walitoa ushahidi kwa njia ya mtandao na hivyo kupunguza gharama na kuimarisha utoaji haki.
Rais Samia ameyasema hayo leo January 3,2025 Jijini Dodoma wakati wa
Maadhimidho ya siku ya Sheria Nchini huku akiwataka Majaji kutokuwa Miungu watu na badala yake watoe haki bila upendeleo.
Ameeleza kuwa utekelezaji wa dira hiyo utavutia mitaji ya uwekezaji jambo litakalohitaji kuingia mikataba mbali mbali baina ya serikali na sekta binafsi hivyo kutoa Rai kwa sekta zote zinazohusika na haki madai kujiandaa vyema katika kutoa huduma za haki.
Aidha ameeleza kuwa katika miaka ijayo Tanzania inatarajia kushuhudia ongezeko kubwa la shughuli za kibiashara na kiuchumi hali itakayoongeza uhitaji wa huduma za utoaji wa huduma za utoaji haki zinazohusiana na biashara hizo.
Amesema mahakama ya Tanzania itakuwa na mchango mkubwa katika kuiwezesha Tanzania kufikia malengo yake ya maendeleo .
Kwa msingi huo Rais Samia ameitaka mahakama ya Tanzania na mahakama ya Mashauri ya Kodi kuwa wawezeshaji wa shughuli za kiuchumi kwa kutenda haki kwa usawa na kwa wakati.
Kwa upande mwingine amesema Serikali imepokea ushauri uliotolewa na Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi wa kukuza ushirikiano katika kampeni za kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria na ameitaka wizara ya katiba na sheria kuratibu suala hilo.
Aidha ameridhia ombi la wakili huyo la kutaka TLS kuendelea kupatiwa huduma za Msaada wa kisheria kwa wananchi wengi zaidi
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma , amesema kuwa hawawezi kufikia malengo ya dira ya 2050 kama wataishi kwa mazoea,fikra,uzembe,ulalamishi hivyo wanahotqji kubadilika na kukubali kukosolewa.
Awali Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari,amesema kuwa Malengo ya Dira ya Taifa yanaweza kufikiwa endapo kila mwananchi anaweza kupata haki kupitia Taasisi ya Haki madai bila kikwazo chochote .
Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) Boniphace Mwabukusi ameiomba Serikali iweke utaratibu wa kisheria na Sera kwa ushirikishwaji wananchi juu ya dira ya maendeleo ya 2050 pamoja na kuwepo kituo jumuishi cha usuluhishi.
Kaulimbiu Tanzania ya 2050 nafasi ya Taasisi zinazosimqmia haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya maendeleo.