Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini Tamko la kuzindua Toleo la Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu la mwaka 2023 kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma pamoja na Mwakilishi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Kizito Mhagama na Viongozi mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria kwa ajili ya kumbukumbu, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.