Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha Dharura cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutekeleza azimio la Mkutano Mkuu kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Kikao kilichofanyika leo tarehe 19 Januari 2025 katika ukumbi wa NEC maarufu kama White House ambapo Wajumbe wamepitisha jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upande Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.