Na Isri Mohamed

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amelipia tiketi 20,000 kwa ajili ya mashabiki wa Timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kuingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuishangilia timu hiyo kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2025 utakaopigwa leo Oktoba 15, 2025 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Akitoa taarifa hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mgeni rasmi katika mchezo huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Mchezo huo wa Kundi H utachezwa majira ya saa 10:00 jioni ambapo Msigwa amesisitiza licha ya kutolewa kwa tiketi hizo hamasa ya Goli la Mama bado inaendelea.

Mchezo wa awali wa Congo vs Tanzania ulichezwa katika dimba la Stade Des Martyrs uliopo mjini Kinshasa na kumalizika kwa Tanzania kupoteza kwa bao moja kwa Nunge.

Please follow and like us:
Pin Share