Skip to main content
JAMHURI MEDIA
Tunaanzia wanapoishia wengine
Home
Kitaifa
Biashara
Siasa
Uchumi
Kimataifa
Makala
Siasa
Uchumi
MCHANGANYIKO
Michezo
Burudani
Kazi/Ajira
Gazeti La Jamhuri
Sitanii
JAMHURI YA WAUNGWANA
Nyundo ya Wiki
Search
December 7, 2023
Habari Mpya
Rais Samia amfariji mama aliyepoteza watoto wawili na wa tatu hajulikani alipo Hanang
Jamhuri
Comments Off
on Rais Samia amfariji mama aliyepoteza watoto wawili na wa tatu hajulikani alipo Hanang
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji muathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Bi. Salome Elifuraha ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini iliyopo Katesh, Hanang. Mama amepoteza watoto wawili kwenye maafa hayo huku mtoto wa tatu akiwa bado hajapatikana hadi sasa. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika hospitali hiyo ya Wilaya Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Jorodom ambalo limeathirika na Mafuriko pamoja na maporomoko ya matope na mawe Wilayani Hanang mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Rais Samia alijionea uharibifu mkubwa uliotokea na kuwapa pole Waathirika wa maafa hayo na kuwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ndugu Elibariki Naman mkazi wa Jorodom, Katesh ambaye ni muathirika wa Mafuriko yaliyotokea Wilayani Hanang. Ndugu Elibariki alikuwa akielezea jinsi majirani zake walivyopoteza maisha pamoja na makazi yao katika maafa hayo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga akielezea kuhusiana na athari za mafuriko yaliyotokea katika eneo la Jorodom Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia ametembelea eneo hilo Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
Post Views:
287
Previous Post
Serikali yawataka watumishi kujiepusha makampuni ya kausha damu
Next Post
Rais Samia azungumza na waathirika wa mafuriko Hanang
Majaliwa : Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa TMA
Pugu Marathon 2025 awamu ya Tatu Kufanyika Mei 31, mwaka huu
Kliniki ya sheria bila malipo yazinduliwa Kilimanjaro
Gethsemane group Kinondoni yaipua wimbo wa Ni siku yetu
Waziri Kombo awakaribisha wafanyabiashara wa Czech
Habari mpya
Majaliwa : Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa TMA
Pugu Marathon 2025 awamu ya Tatu Kufanyika Mei 31, mwaka huu
Kliniki ya sheria bila malipo yazinduliwa Kilimanjaro
Gethsemane group Kinondoni yaipua wimbo wa Ni siku yetu
Waziri Kombo awakaribisha wafanyabiashara wa Czech
Mbowe akemea lugha chafu kipindi cha kuelekea uchaguzi wa CHADEMA
Dk Biteko ataka mitaala vyuoni iendane na mabadiliko ya teknolojia
‘Filamu ya Royal Tour imeongeza watalii asilimia 183’
Trump kuwafuta kazi watu 1,000
Rais Samia :Tanzania imepiga hatua uboreshaji sekta ya afya nchini
‘Jeshi na M23 wakiuka sheria ya vita’
Trump atia saini agizo la kuiondoa Marekani WHO
Soma Gazeti la Jamhuri Januari 21- 27, 2025
Dk Mpango atoa wito kwa majaji, mahakimu wanawake kutofumbia macho vitendo vya ukatili
TEF yawapongeza Dk Samia, Dk Mwinyi, Dk Nchimbi