Rais Samia Suluhu Hassan akionesha kitabu cha matokeo ya mwanzo ya Sensa na Makazi mara baada ya kutangaza matokeo hayo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo Oktoba 31, 2022. Kushoto ni Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Rais Samia akizindua kitabu cha muongozo wa matumizi ya takwimu ya Sensa na Makazi.
Rais Samia akimkabidhi Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi  kitabu cha matokeo ya mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi baada kuzinduliwa. Zanzibar hivi sasa ina zaidi ya wakazi mil. 1.8.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Albina Chuwa akielezea kuhusu mafanikio ya sensa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akisoma taarifa ya mkoa huo na kutoa shukrani kwa Rais Samia kuupa mkoa huo heshima ya kutangazia matokeo hayo ya sensa.
Sehemu ya wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kushudia Rais Samia akitangaza matokeo hayo.