Rais Samia alitaka JWTZ lijikite kwenye kutumia mbinu za kisayansi
JamhuriComments Off on Rais Samia alitaka JWTZ lijikite kwenye kutumia mbinu za kisayansi
Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) lijikite kwenye kutumia mbinu za kisayansi na teknolojia katika kazi zao ili kudumisha ulinzi na usalama.
Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Saba wa CDF na Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wa mwaka 2023 , uliyofanyika katika kambi ya JWTZ 302 KV Lugalo, jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Januari 2024.