Na Stella Aron, JamhuriMedia, Zimbabwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki mkutano wa 44 wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC) ambapo pia  amekabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC -Organ Troika Summit) ambayo ataiongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Rais Dkt. Samia amekabidhiwa uenyekiti huo leo Agosti 17, 2024 katika Mkutano wa wakuu wa nchi na viongozi wa Serikali wa SADC uliofanyika katika jengo la Bunge la Zimbabwe (New Parliament Building) lililoko katika eneo la kilima cha Mount Hapdeo jijini Harare.

Kabla ya kukabidhiwa Rasmi nafasi hiyo ya uenyekiti wa asasi ya siasa ,ulinzi na usalama ya SADC, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema jana alimpongeza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuendesha nchi kwa misingi ya haki na demokarasia ndio maana ameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hiyo.

Naye Katibu Mtendaji wa SADC Elias Magos amesema kuwa nchi za ukanda wa SADC zimeendela kufanya jitihada za kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuimarika hususan kwa nchi zenye changamoto ya migogoro ya Kivita ikiwemo nchi ya Demkrasia ya Congo DRC.

Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Africa SADC ilianzishwa mwaka 1980 ambapo sasa ina nchi wanachama 16 ikiwa na lengo la kuhakikisha nchi hizo zinashirikiana katika masuala mbalimbali ya kukuza na kuimarisha biashara, uchmi, ulinzi na usalama.

Mwaka huu mkutano huu wa 44 wa SADC umeenda sambamba na kauli mbiu isemayo kukuza ubunifu ili kufungua fursa za ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo kuelekea SADC Yenye viwanda ikiwa ni chachu ya kuongeza uzalishaji utakaochochea kasi ya ukuaji wa uchumi. 

      

Please follow and like us:
Pin Share