Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefuta sherehe za Miaka 61 ya uhuru na kuagiza fedha zote kiasi cha shilingi milioni 960 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo kuelekezwa katika ujenzi wa Mabweni katika shule 8 zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu .
Akitangaza uamuzi huo leo Desemba 5,2022 jijini Dodoma Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Utaribu Mhe. George Simbachawene amesema fedha hizo zitaelekezwa Ofisi ya Rais Tamisemi kusimamia ujenzi huo ili kutatua changamoto za uhaba wa mabweni katika shule hizo.
Waziri Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe hizo zitafanyika kwa njia ya Midahalo na Makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika Wilaya zote hapa nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia.
“Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa,”
Na kuongeza kuwa “Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa,”amesema Simbachawene
Mhe.Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema:- MIAKA 61 YA UHURU: AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU.
Waziri huyo ameongeza kuwa Kauli mbiu hiyo inaonyesha nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya.
Muungano wa Tanzania katika kuimarisha uchumi unaojikita katika maendeleo ya watu kwa kufanya mabadiliko katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kufikisha neema na Maendele