Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi wa Shongo-Mbalizi tarehe 05 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akifungulia maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji safi wa Shongo-Mbalizi katika eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali wakati akizindua Mradi wa Maji safi wa Mbalizi, Shongo-Igale katika eneo la Mbalizi Mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera.
Jengo la afya ya Huduma ya Mama na Mtoto lililopo Meta Mkoani Mbeya ambalo limewekewa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 05 Agosti, 2022.