Rais wa Kenya William Ruto, amelivunja baraza lake la mawaziri na kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa serikali, ikiwa ni sehemu ya hatua anazochukua kufuatia maandamano makubwa ya vijana wa kizazi cha Gen Z.

Akihutubia taifa kupitia televisheni nje ya Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto ameahidi kuunda Serikali mpya ambayo itakuwa imara na yenye ufanisi.

”Kulingana na mamlaka niliyopewa na ibara ya 1,521 na 1,525 B ya katiba na kifungu cha 12 cha sheria ya ofisi ya mwanasheria mkuu, nimeamua leo kuwafukuza kazi mara moja mawaziri wote na mwanasheria mkuu wa Jamhuri ya Kenya.” amesema.

Hata hivyo waziri kiongozi, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, na bila shaka ofisi ya Naibu Rais haitaathiriwa kwa njia yoyote ile katika maamuzi hayo.

Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kusikiliza madai ya wananchi na kwamba atashiriki mara moja katika mashauriano ya kina katika sekta mbalimbali na mirengo ya kisiasa na Wakenya wengine, hadharani na binafsi, kwa lengo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Rais Ruto amesema hilo ni muhimu ili kuharakisha hatua madhubuti za kukabiliana na mzigo wa madeni, kuongeza rasilimali za ndani, kuongeza nafasi za ajira, na pia kupambana na ufisadi.

Please follow and like us:
Pin Share