Hotuba ya leo inakuja wakati huu serikali yake ikiendelea kutuhumiwa kutokana na visa utekaji wa watu, ufisadi na sera za kiuchumi ambazo zimepingwa.
Wiki hii kulikuwa na wito wa kufanyika maandamano kupinga hotuba ya rais Ruto.
Licha ya wito huo wa maandamano, mji mkuu umeonekana kusalia mtulivu tofauti na ilivyokuwa kati ya mwezi Juni na Agosti wakati wa maandamano ya kupinga kuongezeka kwa ushuru.
Wanaharakati wanasema wakazi mjini Nairobi wameogopa kujitokeza kushiriki maandamano hayo kwa hofu ya kukabiliwa kwa nguvu na maofisa wa usalama.
Zaidi ya watu 60 waliripotiwa kuuawa katika maandamano ya awali ambapo baadhi ya watu walipanga waliripotiwa kutekwa baadae.
Mwezi huu, shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch katika taarifa yake lilieleza kwamba polisi waliwateka na kuwatesa n ahata kuwaua watu walioongoza maandamano ya kupinga muswada wa fedha.
Barabara ya kuelekea katika majengo ya bunge imefungwa, maandamano yaliokuwa yamepangwa kufanyika yakikosa.
Hii ni hotuba ya tatu ya Rais Ruto tangu kuchukua madaraka mwaka wa 2022 ambapo alihadi kuwainua raia wenye kipato cha chini.