Na Tatu Saad,JamhuriMedia
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameweka mikakati ya kumaliza tatizo la ajira kwa vijana na wananchi kwa ujumla huko Zanzibar.
Rais amekuwa akiwapa vipaumbele vijana na wananchi wake katika suala la ajira Zanzibar, ameweka mikakati kabambe ya kutokomeza tatizo la ajira Zanzibar.
Mkakati wake wa kwanza ukiwa ni kujenga vyuo vya VETA katika kila wilaya Zanzibar ambavyo vitakuwa vikifundisha aina zote za ufundi stadi.
Mbali na kujenga vyuo hivyo pia wanafunzi watapewa vifaa vya kazi baada ya kumaliza elimu ya ufundi katika vyuo hvyo ili waweze kujiajiri kwa kile walichokisomea.
Akizungumza wakati wa ziara katika ofisi za Gazeti la JAMHURI Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis amesema, kabla ya mkakati huo, Rais ameshajenga masoko madogo madogo katika kila wilaya, ambapo yamewasaidia vijana na wananchi wengine kujiajiri kwa shughuli za kijasiriamali masokoni humo.
Mbeto ameongeza kuwa Rais Mwinyi amekuwa akifanya mambo mengi yaliyo nje ya Irani ya chama kama hivyo kutoa fursa za ajira kwa wananchi wake
Amoongeza kuwa katika muda wa miaka miwili Rais Mwinyi amefanya maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali kama elimu,afya na miundombinu.
Kwa upande wa elimu Rais Mwinyi amefanikiwa kujenga shule tisa zenye jumla ya vyumba 811, huku kwenye sekta ya afya amefanikiwa kujenga hospitali 12, moja ikiwa ya ghorofa lenye uwezo wa kulaza wagonjwa 200.
Katika sekta ya miundombinu Mbeto ameeleza kuwa serikali imefanikiwa kujenga barabara zenye hadhi ya rami huku bado ikiendelea na ujenzi wa barabara na miundombinu mingine hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, Zanzibar yote itakua na barabara zenye kiwango cha lami zenye urefu wa Km 275.
Hamis Mbeto ameeleza siri ya mafanikio hayo makubwa ya Rais Mwinyi ni ushirikiano na mchango mkubwa anaoupata kwa chama chake (CCM).