Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akitembelea ujenzi wa Kituo cha Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo hicho na (kulia kwa Rais ) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Kikosi cha KMKM Commodore Azana Hassan Msingiri na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed.(Picha zote na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Kikosi cha KMKM Commodore Azana Hassan Msingiri akitowa maelezo ya Kituo cha Wajasiriamali Tumbe, wakati akitembelea Ujenzi huo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo, na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohammed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisoma maelezo ya Jiwe la Msingi la Kituo cha Wajasiriamali Tumbe Wilaya ya Micheweni Pemba, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo hicho akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo.
Muonekano wa milango ya maduka katika Kituo cha Wafanyabiashara na Wajasiriamali  Tumbe kilichowekwa Jiwe la Msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kikiwa na Milango ya Maduka 54