Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi .Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makaazi Zanzibar Balozi.Mohammed Hamza, kabla ya kuaza kwa zoezi lililofanyika katika Makazi ya Rais Ikulu Ndogo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2022, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar (hawapo pichani) baada ya kumaliza zoezi la kuhesabiwa la Sensa ya Watu na Makazi lililofanyika leo 23-8-2022, katika makazi yake Migombani Ikulu Ndogo Wilaya ya Mjini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Zanzibar Balozi Mohammed Hamza na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa, baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhesabiwa la Sensa ya Watu na Makazi lililofanyika katika makazi yake Migombani Ikulu Ndogo leo 23-8-2022.(Picha na Ikulu)