Na Brown Jonas, JamhuriMedia, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameridhia ushauri wa kuubadili jina uwanja wa Amaan na kuitwa “New Amaan Sports Complex” wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya Uwanja huo uliofanyika Desemba 27, 20203 kisiwani humo
Rais Mwinyi ameridhia ushauri huo uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro alipokua akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuufanya uwanja huu kuwa wa kisasa na wenye viwango vya Kimataifa, mimi naomba niubadilishe jina uitwe New Amaan Stadium” alisema Dkt. Ndumbaro.
Hafla ya uzinduzi wa uwanja huo ilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo muziki na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki baina ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars” na Timu ya Mpira wa Miguu ya Zanzibar “Zanzibar Heros ambazo zilitoka sare ya bila kufungana.