Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi mbalimbali zinazowahudumia mahujaji wanaokwenda Makka, Saudia Arabia kutekeleza ibada ya hijja baada ya kukamilika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Ameyasema hayo leo tarehe 22 Aprili 2023 alipohutubia Baraza la Eid -El-Fitr kwenye ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Alhaj Dk.Mwinyi amewasihi jamii kuendelea kupiga vita mambo yasiyoendana na maadili, mila ,silka na tamaduni za Wazanzibari ili kupata kizazi kilichoongoka.

Akizungumza suala la maadili wakati huu wa Sikukuu ya Eid El Fitr, Rais Alhajj Dk.Mwinyi ameihimiza jamii kuendeleza maadili kwa kujiepusha na vitendo viovu vikiwemo uvunjifu wa amani, udhalilishaji,rushwa , ubadhirifu na dhulma.

Please follow and like us:
Pin Share