Rais Mstaafu wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho, yuko mjini Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Afya na Elimu kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Harvard  (Harvard Ministerial Leadership Program)  inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard. Mheshimiwa Dkt. Kikwete ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu wanoshiriki kutoa mafunzo hayo.

Akiwa Boston, Dkt. Kikwete amekutana na baadhi ya wanafunzi Watanzania wanaosoma hatua mbalimbali za elimu hapo katika Chuo Kikuu cha Harvard.

Please follow and like us:
Pin Share