Rais Dkt. Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwl. Julius Nyerere kilichopo Kibaha, Pwani.


Chuo hicho kinajengwa kwa gharama ya Sh. Bil 100, kwa ufadhili kutoka chama cha CPC cha China kwa ajili ya vyama 6 vya ukombozi Africa (CCM, ANC, ZANU-PF, Frelimo, MPLA na SWAPO na kitachukuwa miaka miwili mpaka kukamilika kwa ujenzi.


Katika hotuba yake rais Magufuli amesema Chuo hicho kitasaidia kuzalisha akina Nyerere, Mandela, Mugabe na wengine wengi, kuanzishwa kwa chuo hicho ni kwa ajili ya kuleta ukombozi wa maendeleo kwa kushirikiana pamoja na kisiwe chuo cha ubaguzi kiwe dira ya waafrika wote.


Pia rais Magufuli amemuomba Mkuu wa mkoa na watu wanaohusika na barabara basi waangalie hill.
“Maana haiwezi badala ya Chuo kukamilika watu kutembea na barabara ya vumbi hadi hapa, nitashangaa sana” Alisema rais Magufuli.