Kamati ya Tuzo za Mandela huko Afrika Kusini zimempa Rais John Magufuli Tuzo ya Amani ya Mandela ya Mwaka 2017 ikiwa ni kutambua jitihada zake katika kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.
Tuzo hiyo ya amani ya Mandela ilikuwa inawaniwa na watu zaidi ya 5000 lakini kamati ya tuzo hiyo ikamchagua Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mwaka huu.
Tofauti na Rais Magufuli viongozi wengine walioshinda ni Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ameshinda Tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na mchango wake wa kukuza Demokrasi nchini mwake.
Wengine ni Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza ambaye amepewa Tuzo ya Ujasiri, Rais Idriss Deby Itno wa Chad ameshinda tuzo ya Ulinzi huku Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zikipewa Tuzo za Ujasiri.
Mandela Peace Prise hutolewa kila mwaka kwa viongozi na watu mbalimbali waliotoa mchango mkubwa katika maeneo mbalimbali kama ujasiri, Amani, demokrasia na ulinzi.