Kufuatia vifo vya Wanajeshi 14 wa Tanzania ambao walikuwa miongoni mwa wanasheshi wa Umoja wa Mataifa UN wa kulinda Amani nchini DRC Congo (MUNUSCO), Amiri Jeshi Mkuu, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein Ally Mwinyi.
Taarifa zinaeleza kuwa Wanajeshi wa Tanzania waliofariki ni 14 Waliojeruhiwa ni 44 na ambao bado hawajulikani walipo ni 2.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Taifa Bw Antonio Guterres ametoa pole
kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wawaathirika kwa tukio hilo na kuwaombea wajeruhi wapone haraka.
kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF). ADF inashukiwa kuhusika na shambulizi kubwa dhidi ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa MONUSCO jioni ya Alhamis Disemba 7, 2017 Bonde la Semuliki, Beni, Kivu Kaskazini, DRC.