Wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar:
1. Dk. Salim Ahmed Salim
2. Fatma Said Ali
3. Omar Sheha Mussa
4. Raya Suleiman Hamad
5. Awadh Ali Said
6. Ussi Khamis Haji
7. Salma Maoulidi
8. Nassor Khamis Mohammed
9. Simai Mohamed Said
10. Muhammed Yussuf Mshamba
11. Kibibi Mwinyi Hassan
12. Suleiman Omar Ali
13. Salama Kombo Ahmed
14. Abubakar Mohammed Ali
15. Ally Abdullah Ally Saleh
Uongozi wa Sekretarieti:
1. Assaa Ahmad Rashid – Katibu
2. Casmir Sumba Kyuki – Naibu Katibu
Rais alisema tarehe ya kuanza kazi kwa Tume hiyo itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadaye kuapishwa.
Alisema kazi hiyo itafanywa ndani ya mwezi huu wa Aprili. Kisheria inatakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18. Alikiri kuwa kazi ya kupata majina ya wajumbe hao ilikuwa ngumu kutokana na wadau kupeleka majina zaidi ya 550.
“Kazi haikuwa rahisi, majina yalikuwa mengi kutoka makundi mbalimbali ya watu, nashukuru kuona kuwa wadau waliitikia vizuri sana, lakini nafasi ni chache. Uamuzi wetu wa kuwataka wadau wapendekeze majina ulikuwa mzuri, na kwa kweli yameletwa majina ya watu makini sana. Majina yote yaliyopendekezwa yalitosheleza mahitaji.
“Hata hivyo hatukuridhisha wadau wote. Kubwa ni kwamba wote watasikilizwa, wanachotakiwa kufanya ni waende kujipanga kutoa maoni yao,” alisema.