Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates kutoka Marekani Dkt. Anita Zaidi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Viongozi mbalimbali kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kimataifa ya The Global Goalkeepers Award kutoka Taasisi ya Gates ya Marekani. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari, 2025.